VIDEO: Dk Tulia aibuka mshindi ubunge Mbeya Mjini

Muktasari:

  • Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Tulia Ackson ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

Mbeya. Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Tulia Ackson ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.
Dk Tulia ameshinda kwa jumla ya kura 75, 225 na kuibuka kidedea dhidi ya wagombea wengine watano wa vyama vya upinzani akiwamo mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu "Sugu" ambaye amepata kura 37, 591.


Wagombea wengine ni Protas Mgaimbila wa Chaumma aliyepata kura 236, Mwakaje Kaili (NCCR-Mageuzi) kura 206 na Rafael Ngonde (CUF) aliyepata kura 88.


Matokeo yametangazwa na Msimamizi Mkuu wa Jimbo la Mbeya Mjini, Amede Ng'wanidako leo Alhamisi Oktoba 29, 2020 katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.