VIDEO: Majaliwa: Ukiugua corona utalazwa palipoandaliwa bila kujali cheo chako

VIDEO: Majaliwa awaondoa hofu watanzania kuhusu huduma karantini

Muktasari:

Waziri Mkuu wa Tanzania,  Kassim Majaliwa amesema mtu yeyote akithibitika kuwa na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19) atapelekwa eneo lililoandaliwa bila kujali cheo chake.

Dodoma. Waziri Mkuu wa Tanzania,  Kassim Majaliwa amesema mtu yeyote akithibitika kuwa na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19) atapelekwa eneo lililoandaliwa bila kujali cheo chake.

Majaliwa ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma leo Jumatano Aprili Mosi, 2020 wakati akisoma hutuba ya mapitio ya mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/21.

“Mtu yeyote atakayebainika kuwa na ugonjwa huo kutangazwa ni lazima bila kujali cheo chake. Awe waziri, katibu mkuu au mkurugenzi atalala palipoandaliwa. Hivyo, niwatake Watanzania kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo,” amesema Majaliwa.

Amewataka Watanzania kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya na Serikali kwa kuwa Tanzania na dunia inapitia kipindi kigumu.

Amewataka wananchi kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuhusu ugonjwa huo.