VIDEO: Mkanganyiko msamaha kwa wahujumu uchumi

Wednesday October 2 2019

DPP,Watuhumiwa wa makosa ya kuhujumu uchumi ,mwananchi habari, gazeti mwananchi, Ikulu, DPP Mganga,

 

By Elias Msuya, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Watuhumiwa wa makosa ya kuhujumu uchumi wanaweza kufurahia wito wa kukiri makosa, kurejesha fedha na hatimaye kupata msahama unaowaepusha na kifungo, lakini wanasheria wananusa ukiukwaji wa sheria na Katiba katika mchakato huo.

Hali kadhalika wanasheria hawakubaliani na kitendo cha Mwendesha Mashtaka Mkuu (DPP), Biswalo Mganga kwenda kwa Rais na nyaraka za watuhumiwa na baadaye kuomba muda wa msamaha uongezwe, wakisema kinakiuka sheria iliyounda ofisi yake.

Walisema hayo wakati Mwananchi ilipotafuta maoni yao kuhusu msamaha uliotolewa na Rais John Magufuli kwa watu wote walioshtakiwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi iwapo watakiri makosa na kukubali kurejesha fedha wanazotuhumiwa kuhujumu.

Baadhi ya wanasheria wamesema suala hilo linaonyesha kuwa DPP ameingiliwa na wengine wamesema jambo hilo ni sahihi.

Mwananchi ilipomtafuta DPP na kumuuliza kuhusu madai kuwa anaingiliwa, alitaka suala hilo lisigeuzwe la kisiasa.

“Ameingiliwa wapi? Acheni siasa na huwa nasema acheni siasa. Lile suala si la kisiasa, kwa hiyo huyo mwanasheria anayesema (hivyo) hajui sheria inasemaje,” alisema Mganga.

Advertisement

Juzi akiwa Ikulu, DPP Mganga alisema jumla ya watuhumiwa 467 wamejitokeza kuomba msamaha na kuahidi kurejesha zaidi ya Sh107 bilioni na pia akaomba kuongezewa siku tatu ili watu zaidi wajitokeze, lakini Rais Magufuli akaongeza siku saba.

Soma zaidi Gazeti la Mwananchi, #Jumatano, Oktoba 2, 2019


Advertisement