VIDEO: Watoto wa bilionea Msuya wahofia kuporwa mali, waomba msaada

Mtoto wa bilionea Msuya, Kelvin Msuya akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akidai kuzuia kuingia katika nyumba ambazo ni mali za marehemu baba yao. Picha na Mussa Juma

Arusha. Watoto watatu wa bilionea Erasto Msuya, aliyeuawa mwaka 2013 kwa kupigwa risasi wameomba msaada kuokoa mali za mabilioni ya fedha za baba yao, wakidai kuna mpango wa kuwanyang’anya.

Wamezitaja mali hizo za Msuya, ambaye alikuwa mchimbaji maarufu wa madini ya Tanzanite kuwa ni nyumba za kifahari, Hoteli ya SG Resort, migodi ya madini na magari.

Msuya, aliyekuwa akimiliki vitegauchumi kadhaa jijini Arusha, aliuawa kwa risasi za bunduki ya kivita aina ya Sub Machine Gun (SMG) Agosti 7, 2013 katika eneo la Mijohoroni wilayani Hai.

Katika eneo la tukio, kuliokotwa maganda ya risasi 22 huku gari ya marehemu aina ya Range Rover namba T800 CKF, bastola na simu zake mbili zikikutwa eneo hilo la tukio.

Kelvin Msuya, mtoto mkubwa wa bilionea huyo, alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari jana kuwa tangu baba yao auawe mwaka 2013 na baadaye mama yao, Miriam Mrita kukamatwa kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha shangazi yao, Anethe Msuya maisha yao yamekuwa ya tabu.

Kwa undani zaidi soma Gazeti la Mwananchi Oktoba 17, 2019.