Vitakasa mikono vya daladala Dar kupokewa kesho

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kesho Alhamisi Aprili 16, 2020 atapokea vitakasa mikono vitakavyotumika katika wa daladala za Mkoa huo.

Dar es Salaam.  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kesho Alhamisi Aprili 16, 2020 atapokea vitakasa mikono vitakavyotumika katika wa daladala za Mkoa huo.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatano Aprili 15, 2020 wakati akizungumza na Mwananchi lililotaka kujua mchakato wa ugawaji wa vitakasa mikono hivyo ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuhakikisha wananchi wanajikinga na maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

Aprili 8, 2020 mfanyabiashara, Rostam Aziz alitoa msaada wa Sh1 bilioni kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kununua vitakasa mikono.

Vitakasa mikono hivyo vitatumiwa na wasafiri  wa daladala wa Dar es Salaam na Zanzibar kabla ya kupanda usafiri huo ili kujikinga na maambukizi.

Katika maelezo yake leo Makonda amesema, “kesho saa tatu asubuhi nitavipokea vitakasa mikono.”

Wakati Makonda akieleza hayo, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid amesema bado hawajapatiwa fedha na kwamba wanazisubiri kwa ajili  ya mchakato.