Wabunge Uingereza wamkalia kooni Boris

Thursday September 12 2019

 

London, Uingereza. Wabunge wa vyama vya upinzani nchini Uingereza wamemtaka Waziri Mkuu, Boris Johnson atangaze kufunga Bunge la nchi hiyo.

Umuzi huo unafuatia mahakama ya juu nchini Scotland kuamua kwamba hatua aliyoichukua ya kusimamisha shughuli za Bunge ilikwenda ikinyume cha sheria.

Jumatano iliyopita mahakama hiyo ilitoa hukumu lakini haikuamuru kubatilishwa kwa hatua ya kusimamishwa Bunge.

Katika kuhumu yake, mahakama hiyo ilisema uamuzi wa mwisho unapaswa kupitishwa na mahakama ya juu ya Uingereza ambako suala hilo litaanza kusikilizwa Jumanne ijayo.

Awali mbunge wa chama cha Scottish National, SNP Joanna Cherry alisema uamuzi huo ni ujumbe kwa Waziri Mkuu Boris kwamba hawezi kuvunja sheria bila ya kuwajibishwa.

Waziri kivuli wa masuala ya Brexit, Keir Starmer alisema hatua ya kulisimamisha Bunge ilikuwa ya makosa. Katika mahojiano na Shirika la habari la BBC Boris alisisitiza kwamba mapumziko hayo ya bungeni ni kwa ajili ya kujiandaa kutoa vipaumbele katika sekta za elimu, huduma za afya na usalama katika vikao vijavyo vya tasisi hiyo.

Advertisement

Advertisement