VIDEO: Wafungwa 79 gereza la Butimba waachiwa huru

Muktasari:

Siku moja baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kuwasamehe wafungwa 5,533 katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, wafungwa 79 kati ya hao waliokuwa wamefungwa katika gereza la Butimba Mkoa wa Mwanza wameachiwa leo Jumanne Desemba 10, 2019.


Mwanza. Siku moja baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kuwasamehe wafungwa 5,533 katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, wafungwa 79 kati ya hao waliokuwa wamefungwa katika gereza la Butimba Mkoa wa Mwanza wameachiwa leo Jumanne Desemba 10, 2019.

Rais Magufuli alitangaza msamaha huo katika maadhimisho hayo, akibainisha kuwa idadi hiyo ni kubwa kuwahi kutokea kuliko wakati mwingine wowote na kutaka walengwa ndio waachiwe.

Katika mkoa wa Mwanza wafungwa watakaopata msamaha huo ni 191.

Leo mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amefika katika gereza la Butimba kwa ajili ya kushuhudia utekelezaji wa agizo la Magufuli huku mkuu wa gereza hilo, Hamza Hamza akitaja idadi ya watakaoachiwa.

"Wafungwa wengine ni wahamiaji haramu ambao wataachiwa huru lakini kwa kufuata taratibu za idara ya uhamiaji,” amesema Hamza.