Waitara ataka wamachinga jijini Mwanza kuhamishiwa soko la Mbugani

Wednesday February 19 2020

 

By Mgongo Kaitira na Johari Shani, Mwananchi [email protected]

Mwanza. Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara ameagiza wamachinga wanaofanya shughuli zao katika maeneo ya watembea kwa miguu na juu ya mitaro jijini Mwanza kuondolewa, kupelekwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili yao.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Februari 19, 2020 alipowatembelea wamachinga wa soko la Makoroboi ambao Februari 12, 2020 walipata hasara baada ya moto kutekeleza baadhi ya vibanda yao.

Mwita amemtaka mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,  Dk Philis Nyimbi kuwapeleka wafanyabiashara hao katika soko la Mbugani.

Vibanda 65 vinavyomilikiwa na wamachinga 159 viliteketea kwa moto na kusababisha hasara ya Sh246 milioni.

Naye Dk Nyimbi ameahidi kuanza kutekeleza maagizo hayo kwa kuwahamisha.

Advertisement