Wake wa Rooney, Vardy wapeana vidonge Instagram

Wednesday October 9 2019

 

London, Uingereza (AFP). Coleen Rooney anasema kuna mtu ametumia akaunti ya Instagram ya Rebekah Vardy kuvujisha habari zinazomuhusu wakati mgogoro unaotokana na mtandao wa kijamii wa Twitter baina ya wake hao wawili wa wanasoka ukitingisha Uingereza.

Coleen, ambaye ni mke wa mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa England Wayne Rooney, aliwaambia wafuasi wake milioni1.3 kwamba ametumia miezi mitano akijaribu kumjua mtu aliyekuwa akisambaza habari zinazohusu maisha yake ya faragha katika mitandao ya kijamii.

Alisema kuwa alibaini kuwa habari hizo zilikuwa zinatoka kutoka katika akaunti ya Rebekah Vardy, nyota wa vipindi vya mazungumzo vya televisheni na ambaye ni mke wa mshambuliaji nyota wa klabu ya Leicester City na timu ya taifa ya England, Jamie Vardy.

Aliandika katika ukurasa wa Twitter akisema: "Kwa miaka michache sasa mtu mmoja wmbaye nilimuamini awe mfuasi wangu kwenye akaunti yangu binafsi ya Instagram amekuwa akiitaarifu gazeti la The SUN kuhusu ujumbe wangu binafsi na habari nazozipandisha.

"Kumekuwa na taarifa nyingi walizopewa kuhusu mimi na familia yangu -- zote hizo bila idhini yangu."

Coleen, 33, alisema alikuwa na hisia ya nani anaweza kuwa na akamblock kila mtu kuona ukurasa wake isipokuwa akaunti inayomilikiwa na ,le wa Vardy.

Advertisement

Alisema alikuwa akiweka ujumbe kadhaa wa habari feki, akisema baadhi zilichapishwa na gazeti la The SUN.

"Nimehifadhi na kupiga picha habari zote halisi ambazo zinaonyesha vizuri kuwa ni mtu mmoja tu aliziona," salisema.

"Ni akaunti ya Rebekah Vardy."

Naye Rebekah alijibu katika akaunti yake ya Twitter akisema: "Kama unadhani hili lilikuwa linatokea ungeniambia na ningeweza kubadili neno la siri kuona kama jambo hilo kama lingeendelea.

"Kwa miaka kadhaa watu tofauti walikuwa wanaweza kuingia kwenye akaunti yangu ya Insta na ni wiki hii tu nilibaini nilikuwa na wafuasi nisiowajua na mwenyewe sikuwahi kuwafuata."


Advertisement