Wanachama wanaotengeneza makundi ya urais CUF waonywa

Muktasari:

  • Naibu katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),  Faki Suleiman amesema chama hicho hakitamvumilia mwanachama atakayetengeneza makundi kwa ajili ya kuwania urais Zanzibar kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Unguja. Naibu katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),  Faki Suleiman amesema chama hicho hakitamvumilia mwanachama atakayetengeneza makundi kwa ajili ya kuwania urais Zanzibar kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Ametoa kauli hiyo jana Jumapili Agosti 25, 2019 katika mahojiano na Mwananchi.

Amebainisha kuwa siku za hivi karibuni baadhi ya watu wanasambaza taarifa katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwagombanisha viongozi wa chama hicho, jambo alilodai kuwa halivumiliki.

Amesema wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali ndani ya CUF wanatakiwa kufuata taratibu si vinginevyo.