Wanafunzi 90 washindwa kumaliza kidato cha nne kwa sababu ya utoro, mimba

Muktasari:

Wanafunzi 90 wa shule ya sekondari Maisome halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wameshindwa kumaliza kidato cha nne mwaka 2020 kutokana na utoro na kupata ujauzito .

Buchosa. Wanafunzi 90 wa shule ya sekondari Maisome halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wameshindwa kumaliza kidato cha nne mwaka 2020 kutokana na utoro na kupata ujauzito .

Walioanza kidato cha kwanza walikuwa 147 ambapo wavulana walikuwa 89 na wasichana 58 lakini ni 55 tu ndio waliohitimu kidato cha nne. Kati ya waliohitimu 26 walikuwa wavulana na 29 wasichana ambao wanne kati yao wakipata ujauzito.

Akizungumza jana Ijumaa Oktoba 16, 2020 katika mahafali ya shule hiyo amesema changamoto kubwa inayowakabili ni wanafunzi wengi kushindwa kuhitimu kidato cha nne baada ya kupata mimba na wengine kutohudhuria masomo kwa muda mrefu.

"Naomba jamii pamoja na wazazi kujitolea kujenga bweni kuwasaidia watoto wa kike na kuwaepusha na vishawishi,” amesema Magadula.

Mmoja wa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo, Faustine Bizo amesema umbali mrefu, vishawishi ndiyo sababu wanafunzi wengi kushindwa kuendelea na masomo yao.