Jengo la darasa laanguka Kenya, wanafunzi saba wafariki na kujeruhiwa

Muktasari:

Jengo la darasa la Shule ya Precious Talent limeanguka leo asubuhi nchini Kenya na kusababisha vifo na majeruhi kwa wanafunzi.

 

Dar es Salaam. Wanafunzi saba wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya jengo la darasa la Shule ya Precious Talent kuanguka eneo la Ngado Nairobi nchini Kenya saa 1 asubuhi leo Jumatatu Septemba 23, 2019.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu nchini humo imesema shughuli ya uokoaji inaendelea na wanafunzi wanne wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta.

Mmoja wa wazazi katika eneo hilo amesema ajali hiyo inaweza kuwa imesababishwa na uchimbaji wa mfumo wa kupitisha maji taka karibu na shule hiyo.