Wananchi India waandamana kupinga ubakaji wa wanawake

Tuesday December 3 2019

India. Wabunge nchini India wameshinikiza kuchukuliwa kwa hatua zaidi dhidi ya wahalifu waliohusika kumbaka na kumuua mwanamke mmoja.

Aidha, mamia ya wananchi nchini humo wameandamana nchi nzima wakitaka uchunguzi wa tukio hilo ufanyike mara moja.

Waandamanaji hao waliokuwa na mabango yaliyokuwa yakishinikiza uchunguzi wa haraka walikusanyika katika eneo la karibu na Bunge mjini New Delhi leo Jumanne Desemba 3.

Ijumaa iliyopita, wanaume wanne weye umri kati ya miaka 20 na 25 walikamatwa kwa tuhuma za kumbaka na kumuua mwanamke huyo ambaye ni daktari wa wanyama.

Tuukio hilo linadaiwa kutokea karibu na mji wa Hyderabad uliopo Kusini mwa nchi hiyo.

Inaelezwa kuwa mabaki ya mwili wa mwanamke huyo yalipatikana siku tatu baada kutoweka nyumbani kwake Jumatano iliyopita.

Advertisement

Polisi nchini India kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ilisema kuwa mwanamke huyo alinyongwa kabla ya mwili wake kuchomwa moto.

Wakizungumzia tukio hilo, wabunge wameeleza kusikitishwa na ongezeko la vitendo vya kihalifu dhidi ya wanawake.

Wabunge hao walisema kitendo hicho kinahashiria hali ya usalama wa wanawake wa Taifa hilo iko shakani na kutaka mamlaka husika kuchukua hatua kali kwa wote waliohusika na unyama huo.


Advertisement