Wanandoa raia wa China waliokiri kumpa Sh11 milioni bosi TRA wahukumiwa kulipa faini

Muktasari:

  • Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ronglan Intl Industry and Trade Co. Ltd, Zheng Rongman (50) na mkewe Ou Ya (47), kulipa faini ya Sh1 milioni kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kutoa rushwa ya Sh11.5 milioni kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk Dk Edwin Mhede.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ronglan Intl Industry and Trade Co. Ltd, Zheng Rongman (50) na mkewe Ou Ya (47), kulipa faini ya Sh1 milioni kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kutoa rushwa ya Sh11.5 milioni kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk Dk Edwin Mhede.

Kwa mara ya kwanza wanandoa hao walifikishwa katika mahakama hiyo jana Jumanne Februari 25, 2020 kujibu shtaka hilo na kesi hiyo ilipangwa kuendelea leo kwa ajili ya kusomewa maelezo yao.

Mbali na kupigwa faini  mahakama hiyo imetaifisha Sh11.5milioni na kuwa mali ya Serikali.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Februari 26, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakamani hiyo, Huruma Shaidi baada ya washtakiwa hao  kutiwa hatiani kwa kosa la kutoa rushwa.

Rongman na Ya, ni raia wa China na wakazi wa Kinyambo, wilaya ya Mafinga mkoani Iringa.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi