Wanane wajitosa Bavicha kumrithi Sosopi

Muktasari:

Wanachama wanane wa Chadema wamejitosa kugombea uenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha) katika uchaguzi utakaofanyika Desemba 9, 2019.

Dar es Salaam. Wanachama wanane wa Chadema wamejitosa kugombea uenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha) katika uchaguzi utakaofanyika Desemba 9, 2019.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Desemba 3, 2019 katibu mkuu wa baraza hilo, Julius Mwita amesema waliochukua fomu na kurejesha kuwania nafasi ya mwenyekiti wa sasa Patrick Ole Sosopi anayemaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ni Lusako Mwamwile, John Pambalu, Mdude Mpaluka, Mathayo Gekul.

Wengine ni Dorcas Mwilafi,  Mhere Mwita, Albert Alphonce na Yuda Gueti.

Amesema watakaogombea umakamu mwenyekiti wa baraza hilo ni Moza Mushi, Ester Fulano, Francis Garatwa, Mohania Mwita na upande wa Zanzibar ni Ombari Nasoro Othaman, Rukia Aboubakari Mohamed na Habibu Khamis.

Mwita amesema nafasi ya katibu mkuu watakaogombea ni Gwamaka Mbughi, Nusrat Hanje, Edward Simbeye, Chacha Machera, Noel Shayo, Innocent Kisanyage, Ali Hamedi, Titho Kitalika na Amos Ntobi.

Unaibu katibu mkuu bara ni Sunday Urio, Hilda Newton,  Juliana Chogga, Juvenal Shirima,Yohana Kaunya, Justine Saimon, Philimon Mwanjala na Ayub Migera. Watakaowania nafasi hiyo kwa upande wa Zanzibar ni  Haji Abeid Haji na Thuaiba Ali Khamis.

“Nafasi ya uhamasishaji ni Twaha Mwaipaya, Lumola Kahumbi, Enock Chaulema na Denis Ngonyani. Mweka hazina waliojitokeza ni Lilian Paul, Nice Gisente na Catherine Kessy,” amesema Mwita.