Wanaume 4.4 milioni wavuliwa mikono ya sweta

Sunday December 1 2019

 

By Waandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Mwanza. Zaidi ya wanaume 4.4 nchini Tanzania wametahiriwa katika kipindi cha miaka miwili ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya kupambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

Hayo yameelezwa leo Jumapili Desemba Mosi, 2019 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akibainisha kuwa wamefanyiwa tohara katika kampeni  iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2017 hadi Septemba, 2019.

"Utafiti wa kitaalam na kitabibu unathibitisha kuwa tohara kwa wanaume inapunguza maambukizi ya VVU kwa karibu asilimia 60," amesema.

Baadhi ya Mikoa ambayo imefanyika tohara hiyo ni Mwanza, Geita, Manyara, Arusha, Shinyanga, Kagera, Simiyu na Morogoro.

Advertisement