Waomba kumaliza kesi nje ya mahakama

Muktasari:

  • Washtakiwa kesi ya Katani limited sasa wameandika barua kuomba kesi majadiliano ya nje ya Mahakama

Tanga. Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga imetaarifiwa juu ya nia ya washtakiwa wa kesi ya uhujumu uchumi ya Katani Limited kuomba kuiondoa kesi hiyo mahakamani na kujadiliana nje ya mahakama.


Mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi, Ruth Mkisi kesi hiyo ilipoletwa kwa ajili ya kutajwa kesi wakili wa washtakiwa hao wawili Warehema Kibaha aliiambia mahakama hiyo kwamba Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali imepelekewa barua ya maombi hayo, lakini bado haijajibu.


Baada ya kusikilizwa maombi hayo ya washtakiwa, Hakimu Mkisi aliahirisha shauri hilo hadi Mei 05, 2020 litakapotajwa tena na washtakiwa wote wawili wamerudishwa rumande.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi ya mwaka 2019 iliyowahusu washtakiwa watatu, Salum Shamte, Juma Shamte na Fatuma Diwani, mshtakiwa wa kwanza alifariki dunia wiki iliyopita na hivyo kubaki washtakiwa wawili.