Warembo Top Model ni nani?

Friday October 18 2019

Akina nani ni warembo bora ambaop walivutia kila mtu wakati wa maonyehso ya mavazi ya hivi karibuni? Kunahitajika muhtasari.
Kwanza kabisa, habari mpya ambayo imesambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii: warembo wawili, Bella Hadid na Kendall Jenner wote sasa wana nywele za blonde. Hii ni habari muhimu sana hasa kwa kuzingatia nguvu yao na kuwa na wafuasi wengi katika akaunti zao za mitandao ya kijamii. Pia wameonyesha pamoja mavazi ya Burberry jijini London, wakiozungukwa na warembo wenginer wengi.
Pia ni kweli kwamba msimu huu umetawaliwa na kuonekana kwa mrembo Bella Hadid katika maonyesho kadhaa ya mavazi, si mbali sana na dada yake Gigi, ambaye kuonekana kwake mara nyingi hufurahisha watu.
Msichana mwingine ambaye aliacha alama katika maonyesho hayo ya mavazi ni Adut Akech. Mikogo yake katika kutembea, mwonekano na macho yake yalifurahisha tena wabunifu wengi wa mavazi, akiwemo Pierpaolo Piccioli, hadi akawa msichana wa kwanza mweusi kutumiwa kutangaza manukato ya Valentino.
Adut Akech ni mfano wa diversity. Mtu anaweza kusifu kuwepo kwa wanawake warembo tofauti jukwaani, jambo ambalo lilianzishwa katika maonyesho yaliyopita.
Ukizungumzia wasichana waliovutia msimu huu; tulipenda kumuona IRINA SHAYK katika maonyesho ya London na Milan, AMBER VALLETA katika maonyesho ya STELLA MCCARTNEY na ISABEL MARANT, na hatuwezi kumaliza muhtasari huu wa maonyesho ya mavazi bila ya kutaja kuonekana kwa NAOMI CAMPBELL ambaye alifunga maonyesho ya mavazi yaliyobuniwa na Saint Laurent.
 

Advertisement