Watu 14 waliokuwa wasafiri na ndege iliyoanguka, wabadilishiwa usafiri

Muktasari:

Ndege ya Kampuni ya Auric imeanguka leo asubuhi Jumatatu katika Uwanja wa mdogo wa ndege wa Soronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania na kusababisha vifo vya watu wawili akiwamo rubani wa ndege hiyo.

Ndege hiyo ya kampuni ya Auric air yenye namba 5H-AAM iliyokuwa inaendeshwa na Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania, Venance Mabeyo imepata imeanguka leo Jumatatu asubuhi Septemba 23, 2019.

Katika ndege hiyo kulikuwa na Nelson na Nelson Orutu ambaye inadaiwa ni rubani mwanafunzi lakini si wa kampuni hiyo ambo wote kwa pamoja walifariki ndani ya ndege hiyo iliyoanguka muda mfupi baada ya kuruka kwenda kuwabeba wageni hao waliokuwa Grumeti Kirawira.

Msimamizi wa kampuni hiyo kwa Serengeti,  Peter Kimaro ameiambia Mwananchi kuwa wamebadilisha safari za ndege zao mbili na kwenda kuwachukua wote na kuwapeleka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

"Wageni hao walikuwa wa kampuni ya And beyond Tanzania na sisi tulikodiwa kuwasafirisha, baada ya tukio tukachukua hatua ya haraka maana wale walikuwa na ratiba yao," amesema.

SOMA ZAIDI