Waziri Hasunga kuzindua mkakati wa kuendeleza zao la mpunga awamu ya pili

Sunday December 15 2019

By Elias Msuya, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga kesho Desemba 16 atazindua Mkakati wa kuendeleza zao la mpunga awamu ya pili 2019-2030, jijini Dodoma Tanzania.  

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 15 na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe imesema mkakati huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia 2019/2020 hadi 2029/2030.

“Uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa St Gaspar Jijini Dodoma kuanzia saa 2.00 asubuhi. Wadau wa zao la mpunga na wananchi mnaalikwa,” imesema taarifa hiyo.

Advertisement