Waziri Mpango apendekeza utaratibu wa kuondoa mizigo bandarini

Thursday June 13 2019

kufuta tozo,maduka  vyakula, biashara samaki, mwananchi habari,bunge bajeti, selikali bajeti 2019/2020,  Dk Philip Mpango,

Wabunge wa Viti Maalum (Chadema) wakisoma kitabu cha hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020, ilipokuwa ikiwasilishwa bungeni jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amependekeza kuweka utaratibu mpya wa kuondoa mizigo bandarini ambapo wananchi wa kawaida wataruhusiwa kutoa mizigo yao bila ya kuwa na ulazima wa kutumia Wakala wa Forodha.

Waziri Mpango amesema hayo wakati akiwasilisha makadirio na mapato ya Serikali kwa mwaka 2019/20 leo Alhamisi bungeni jijini Dodoma.

Huku akishangiliwa na wabunge, Waziri Mpango amesema licha ya kuweka utaratibu huo lakini, “hautahusisha mizigo inayopitishwa Tanzania kwenda nje ya nchi.”

“Aidha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaandaa utaratibu wenye kueleweka kwa urahisi ili kuwawezesha Wananchi kugomboa mizigo yao kwa gharama nafuu zaidi na bila kuchelewa,” amesema

 


Advertisement

Advertisement