Wenje achaguliwa tena uenyekiti wa Chadema kanda ya Victoria

Muktasari:

Ezekiah Wenje amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria.

Mwanza. Ezekiah Wenje amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria.

Msimamizi wa uchaguzi huo uliofanyika jana Ijumaa Novemba 29, 2019 jijini Mwanza, Benson Kigaila amesema mbunge huyo wa zamani wa Nyamagana alipata kura 50.

"Amewashinda Chifu Kalumuna aliyepata kura 25 na Tungaraza Njugu aliyepata kura mbili," amesema Kigaila.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Wenje amesema mikakati yake ni kukiimarisha chama hicho kuwa na wanachama wengi zaidi.