Wiki ya Azaki Tanzania yatangazwa

Wednesday September 11 2019

By Asna Kaniki, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Asasi za kiraia nchini Tanzania zimezindua wiki ya Azaki itakayowezesha utambuzi wa maeneo ya ushirikiano na ufanyaji kazi pamoja baina ya watendaji wa Serikali na wa sekta binafsi.

Akizungumza leo Jumatano Septemba 11,2019 katika uzinduzi rasmi wa wiki hiyo, Mkurugenzi wa Asasi za kiraia nchini Tanzania, Francis Kiwangwa amesema wiki hiyo itakayojumuisha washiriki zaidi ya 600, asasi za kiraia zipatazo 400 ili katika kuhakikisha watendaji watakaohusishwa kutoka sekta mbalimbali wanakuwa sehemu muhimu ya ushirikiano kwa lengo la kuleta maendeleo.

Amesema lengo la kuzindua wiki hiyo ya azaki itakayoanza Novemba 4 hadi 8, 2019 yenye kauli mbiu isemayo ‘ubia kwa maendeleo na ushirikiano kama nguzo muhimu kwa maendeleo ya Tanzania ni kuongeza uaminifu kati ya Asazi za kiraia na vyombo vingine vinavyohudumia jamii.’

 

“Wiki hii ni fursa ya kuleta sauti za wananchi kwa pamoja lakini pia kuongeza wigo wa kuwahudumia wananchi katika maeneo mbalimbali chini,” amesema

“Lakini pia katika wiki hiyo tutapokea mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wadau na Serikali sambamba na utoaji tuzo kwa asasi bora ya mwaka,” ameongeza

Advertisement

Kwa upande wake, mwakilishi kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Marion Caussanel amepongeza asasi hizo kwa kuungana na serikali, wadau na wananchi kwa ujumla kufanya kazi kwa pamoja.

 

Advertisement