Kauli ya Ukawa sasa dhahiri bungeni

Wednesday June 22 2016

By Nuzulack Dausen, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Kauli iliyotolewa na wabunge wa Ukawa kuwa watasusa kushirikiana katika kazi za aina yoyote ile na wabunge wa CCM, imedhihirika jana baada ya baadhi yao kususa kusalimiana nao.

Wabunge wa CCM, Richard Ndassa (Sumve) na Kangi Lugola (Mwibara), wameeleza kutojibiwa salamu zao na wabunge hao walipowasalimia.

Advertisement