Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki DR Congo wapigwa marufuku dhidi ya Chile

Muktasari:

  • Mechi hiyo imepangwa kuchezwa leo, Jumanne katika mji wa Orleans nchini Ufaransa.

Mechi ya mwisho ya maandalizi ya Kombe la Dunia ya DR Congo dhidi ya Chile itachezwa bila mashabiki kutokana na wasiwasi kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DR Congo.

Mechi hiyo imepangwa kuchezwa leo, Jumanne katika mji wa Orleans nchini Ufaransa.

Awali ilikuwa ichezwe mjini Cadiz nchini Hispania, lakini Meya wa eneo hilo alisaini amri ya kuzuia mchezo huo kufanyika kama hatua ya tahadhari.

Waandalizi wa Kombe la Dunia nchini Marekani wanahitaji wachezaji na maafisa wa DR Congo kukaa nje ya nchi yao kwa siku 21 bila kuonyesha dalili zozote za Ebola kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini humo.

Hakuna mchezaji wa DR Congo ambaye ametembelea nchi yake hivi karibuni, kwa kuwa wote wanacheza soka katika klabu za nje ya DR Congo. Hata hivyo, baadhi ya maafisa wa timu na mashabiki wamewasili kutoka nchini humo.

Kikosi hicho kwa sasa kinakamilisha maandalizi yake mjini Marbella baada ya kambi ya mazoezi ya siku 10 nchini Ubelgiji, ambapo kilicheza dhidi ya Denmark na kutoka suluhu.

Hii ni mara ya kwanza kwa DR Congo kufuzu Kombe la Dunia tangu mwaka 1974, waliposhiriki kwa jina la Zaire. Wakati huo walimaliza mkiani mwa kundi lao baada ya kufungwa na Scotland, Brazil na Yugoslavia.

Katika Kombe la Dunia lijalo, DR Congo imepanga kuweka kambi yake katika mji wa Houston. Mechi yao ya kwanza ya Kundi K itakuwa dhidi ya Ureno tarehe 17 Juni.

Baadaye watasafiri kwenda Guadalajara nchini Mexico kucheza dhidi ya Colombia kabla ya kurejea Marekani kwa ajili ya mechi dhidi ya Uzbekistan mjini Atlanta.

Mlipuko wa Ebola mashariki mwa DR Congo unasababishwa na aina nadra ya virusi hivyo inayojulikana kama Bundibugyo Ebola.

Kwa sasa hakuna chanjo iliyothibitishwa kwa aina hiyo ya virusi, na WHO imesema kuwa inaweza kuchukua hadi miezi tisa kabla ya chanjo kuwa tayari kutumika.