Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maajabu aliyofanya Tupac ndani ya miaka saba

Muktasari:

  • Kati ya mwaka 1989 hadi 1996, maisha ya Tupac Shakur hayakuwa  ya msanii anayepanda ngazi za mafanikio. Ilikuwa ni simulizi ya kijana aliyebeba ndoto, kipaji na ujasiri wa kusema kile ambacho wengi waliogopa kukisema.

Marekani. Kati ya mwaka 1989 hadi 1996, maisha ya Tupac Shakur hayakuwa  ya msanii anayepanda ngazi za mafanikio. Ilikuwa ni simulizi ya kijana aliyebeba ndoto, kipaji na ujasiri wa kusema kile ambacho wengi waliogopa kukisema.

Kutoka kuwa mwanafunzi wa ushairi na sanaa mjini Baltimore, Tupac alianza kuonekana katika tasnia kama dansa wa kundi la Digital Underground kabla ya kujijengea jina lake mwenyewe.

Ndani ya miaka michache, aligeuka kutoka msanii wa kawaida na kuwa sauti ya kizazi kizima cha vijana waliokuwa wakikabiliana na changamoto za ubaguzi, umasikini na ukosefu wa haki.

Lakini safari yake haikuwa ya muziki pekee. Kila mwaka uliambatana na ushindi wake pamoja na migogoro iliyomweka kwenye vichwa vya habari.

Mwaka 1995 alipokumbwa na matatizo ya kisheria na kufungwa gerezani, wengi walidhani huo ungekuwa mwisho wa safari yake ya muziki. Badala yake, ndipo ukurasa mwingine mkubwa ulipoanza.

Mtendaji wa muziki Suge Knight aliingilia kati na kusaidia kulipia dola milioni 1.4 sawa na Sh3 bilioni dhamana iliyomtoa gerezani kupitia kampuni ya Death Row Records. Makubaliano yalikuwa wazi.

Tupac angelipa gharama hizo kupitia kazi yake ya muziki kwa kurekodi albamu kadhaa chini ya lebo hiyo.

Baada ya kutoka gerezani, Tupac alifanya kazi kwa kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa na wengi. Ndani ya muda mfupi alirekodi nyimbo na albamu zilizotikisa dunia, akionyesha kana kwamba alijua muda wake ulikuwa mdogo.

Kila wimbo, kila mahojiano na kila hatua aliyopiga ilionyesha mtu aliyekuwa na haraka ya kuacha alama ambayo isingefutika.

Kadiri alivyoendelea kutimiza wajibu wake kwa Death Row, alianza kuwaza maisha ya baada ya mkataba huo.


Alikuwa akizungumza kuhusu kujisimamia mwenyewe, kuanzisha miradi yake binafsi na kujenga himaya yake nje ya ushawishi wa wengine. Ndoto yake kubwa ilikuwa kuipa nguvu zaidi familia yake ya kisanii ya Outlawz na kuanzisha njia mpya ambayo angeidhibiti yeye mwenyewe.

Watu waliokuwa karibu naye wanasema katika miezi yake ya mwisho alikuwa na mipango mingi kuliko wakati mwingine wowote katika maisha yake.

Alikuwa akifikiria albamu mpya, filamu, biashara na maisha mapya baada ya kutimiza majukumu yake kwa Death Row. Kwa mara ya kwanza, alionekana kuwa karibu kuanza sura mpya ya maisha yake.

Lakini Septemba 1996, kabla hajatekeleza kikamilifu mipango hiyo, maisha yake yalikatishwa ghafla akiwa na umri wa miaka 25 tu.

Katika kipindi hicho kifupi chini ya Death Row, Tupac alishiriki miradi mikubwa iliyofanikiwa sana duniani, ikiwemo albamu All Eyez on Me (1996), ambayo ilibeba nyimbo kubwa kama California Love, How Do U Want It, 2 of Amerikaz Most Wanted na Ambitionz Az a Ridah.

Pia alikamilisha mradi wa mwisho uliotolewa baada ya kifo chake, The Don Killuminati, The 7 Day Theory, uliohusishwa na jina la Makaveli, ambao pia ulipata mafanikio makubwa sana.