Miss Japan arudisha taji baada kugundulika ana uhusiano na mume wa mtu

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Waandaaji wa taji hilo waligundua kuwa alikuwa akijua kuwa mwanaume anayejihusisha naye kimapenzi ni mume wa mtu, baada ya mwanamitindo huyo kuzungumza ukweli kupitia ukurasa wake wa Instagram jana Jumatatu, Februari 5, 2024.

Japan. Mwanamitindo maarufu kutoka nchini Japani, Karolina Shiino, mzaliwa wa Ukraine ambaye alishinda taji la Miss Japan mwezi uliopita, amejiuzulu nafasi yake baada ya gazeti moja la udaku kuweka wazi kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wa mtu.

Kutokana na kashfa hiyo, mratibu wa shindano hilo alikanusha madai hayo Alhamisi iliyopita akieleza kuwa Shiino hakujua kuwa mwanaume huyo ambaye ni daktari alikuwa mume wa mtu.

Hata hivyo, baadaye waandaaji wa taji hilo waligundua kuwa alikuwa akijua kuwa mwanaume anayejihusisha naye kimapenzi ni mume wa mtu, baada ya mwanamitindo huyo kuzungumza ukweli kupitia ukurasa wake wa Instagram jana Jumatatu, Februari 5, 2024.

Shiino alirudisha taji hilo kwa bodi ya waandaaji wa mashindano hayo na hii inakuwa mara ya kwanza kwa Miss Japan kuachia taji lake baada ya kutangazwa kuwa mshindi Januari 22, 2024.