Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndani ya Boksi: Adui wa Diamond ni Diamond 

Muktasari:

  • Utanielewa kirahisi zaidi kama utatambua kuwa kina Fid Q na wengi wa kitambo, bado wanatoa kazi bora. Lakini hazina matokeo makubwa ‘coz pipo’ washageuza shingo. Wanashughulika na watu wapya hivi sasa.

Dar es Salaam. Kitu pekee kigumu kuelezeka na kinachosisimua moyo. Ni penzi jipya. Ukitaka kuona ujinga wa binadamu ni pale anapokuwa kwenye penzi jipya. Hata mtu upatapo kitu kipya ni rahisi kudharau kile cha zamani.

Utanielewa kirahisi zaidi kama utatambua kuwa kina Fid Q na wengi wa kitambo, bado wanatoa kazi bora. Lakini hazina matokeo makubwa ‘coz pipo’ washageuza shingo. Wanashughulika na watu wapya hivi sasa.

50 Cent ‘alipodrop’ ikawa ngumu kurudi juu. Hata Mond na Alikiba wajiangalie, wanatakiwa kulinda thamani zao. Wadau wa muziki wakiondoa mahaba yao, wataona maisha ya muziki ni ushetani. Na kazi ngumu zaidi maishani.

Muziki ni biashara ya mahaba, mwanamuziki anaweza kuwa na kazi ya kawaida lakini kama watu wanampenda watampokea hivyo hivyo. Wanamuziki wanatakiwa kujitenga na mashindano kama kwenye soka. 

Muziki ni thamani ya msanii, na unaweza kufanya kazi nzuri lakini kama thamani yako kwa watu imeporomoka, utapuyanga. Siku zote mwanamuziki anatakiwa kupambana kulinda soko lake. 

Diamond anajua kumekuwa na kampeni ya wazi na gizani dhidi yake. Kuna watu wanatamani huyu msela wa Tandale siku moja anaporomoka. Tunajua anajua na kutambua na yeye ndiye bingwa wa kuyazua. 

Kwa mafanikio yake, hapendwi na wengi, hivyo popote alipo Mondi hushindanishwa kila mara. Kama siyo Kiba basi Davido. Sababu ni kukerwa na mafanikio ya Mondi.

Mbele ya jamii, Mondi huonekana mjivuni wa mafanikio yake. Kiba yeye kafanikiwa kuiaminisha jamii kuwa yeye ni mnyenyekevu. Ndo maana shabiki ukiulizwa sababu ya kumpenda Alikiba, mara nyingi neno lao ni kwamba  “Jamaa hana makuu”. Utadhani wanamjua kiundani kumbe picha ya nje.

Hakuna mafanikio bila chuki. Ukishachomoza kimafanikio, utachukiwa na unaowajua na usiowajua. Ni vyema kuhakikisha huzalishi maadui kwa kujitakia, coz mafanikio peke yake ni uadui mkubwa. Hili somo lipo kushoto kwa Mondi.

Asili ya binadamu ni sawa na ule msemo wa “aliye juu mngoje chini”. Kama hana namna ya kupanda ili amfikie aliye juu, basi ikiwepo nafasi ya kumshusha, basi atafanya hivyo. Anakuja ule msemo wa “tukose wote.” 

Mondi atajidanganya akiamini wenzake wanampenda. Eti wao wako ‘praudi na kukaa kwake kileleni. Kila mmoja kwa nafasi yake anatamani yeye ndiye awe juu ili apigiwe saluti na tasnia ya muziki Bongo. 

Kuanzia Konde Boy hadi Lavalava na Mbosso. Hakuna binadamu anayependa kuwa wa mwisho, amshangilie mwenzake ambaye anachomoza kama mnara. Huku yeye akiwa hatambuliki. Hakuna kitu kama hicho daima dumu.

Usidhani Ronaldo na Lionel Messi wanapendwa sana na wachezaji wenzao. Kila mtu hutamani kuwa juu.  Mpaka huku mitaani watu hawafurahii kuzidiwa kimaisha na jirani. Ni katika hali hiyo, Mondi yupo kwenye kona mbaya. 

Kwa hali hiyo, Mondi anapaswa kuwa mwangalifu. Neno lake moja linaweza kugeuza asali kuwa kinyesi. Inategemea na wahenga watatafsiri vipi. Wenzake wengi hawampendi Mondi. 

Hakuna sababu zaidi, isipokuwa wanamuona anaringia mafanikio yake. Ingawa ukweli ni kwamba wapo ambao kama wangekuwa wao kama Mond, tunayemuona leo, wangefanya mambo ya ajabu zaidi. Maana hawana nusu ya kile cha Mondi ila huo mvimbo wao?

Ni angalizo kwa Diamond na mtu yeyote mwenye mafanikio sana kimaisha. Unapaswa kuwa makini kwa vitendo na maneno. Maana chochote ukikifanya au kukisema hulinganishwa na mafanikio yake. Huu ni mtihani mkubwa.

Chochote kile atakachofanya au kukitamka chenye ishara fulani ya kujikweza au dharau, kitatafsiriwa kwa mafanikio yake. Ni mtihani mkubwa na huwashinda wengi sana. Sababu asili ya binadamu kubadilika kadiri anapopata mafanikio. 

                   


Hata kama anaweza kujitahidi kujificha lakini kiburi cha siri atakuwa nacho. Kiasili, mtu aliyepata mafanikio makubwa anapojionesha mnyenyekevu mara nyingi huwa ni unyenyekevu wa maigizo. Kimsingi huwezi kuwa mnyonge tajiri wa Afrika.

Hata hivyo, kanuni ni ileile, watu watakupenda, watakupa utajiri kwa kazi zako, lakini hawataki ukifanikiwa uwe na kiburi pamoja na majivuno. Wanapenda uwe mnyenyekevu, mtiifu na mwenye hofu kwao kuliko wazazi na Mola wako. Watu bana. 

Kuna ‘intavyuu’ fulani ya Mr Blue na mtangazaji. Akaulizwa juu ya zile mishe za Mondi. Blue akasema kuwa hakuna kama Diamond. Na akaelezea kwanini hakuna kama Diamond. Akajibu Mondi hutumia akili yake kusaidia wengine.

Mtangazaji akasema hata Alikiba ameshafanya sana hivyo. Kidogo Mr Blue akavuta pumzi na kutoa jibu kamili. Akasema: Diamond anasaidia watu kwa kiwango cha juu mpaka wanakuja kumletea upinzani hata yeye mwenyewe. 

Mtangazaji akaishia kuitikia tu. Yes, Diamond anazalisha watu waje kuwa Diamond. Yes! Mazao yake yanakuwa mazito kuliko wapinzani wake wa mwanzoni. Adui wa Diamond ni Diamond mwenyewe. Ondoka na hili hapa kwa sasa.