Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usichokifahamu uhusika wa Nathan kwenye 'The Boys'

Muktasari:

  • Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa mwigizaji Nathan Mitchell, anayejulikana kama Black Noir katika Filamu ya "The Boys" Season 4 ambayo aliigiza kama mtu mwenye matatizo ya kusinzia 'narcolepsy' lakini katika uhalisia inaelezwa kuwa kweli mwigizaji huyo ana tatizo hilo.

Marekani, Katika ulimwengu wa filamu, wahusika hujulikana zaidi kwa uwezo wao wa kuigiza, lakini wakati mwingine, ukweli wa maisha yao hujitokeza kwenye filamu hizo au wengine hupatiwa uhusika unaofanana na tabia zao.

Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa mwigizaji Nathan Mitchell, anayejulikana kama Black Noir katika Filamu ya "The Boys" Season 4 ambayo aliigiza kama mtu mwenye matatizo ya kusinzia 'narcolepsy' lakini katika uhalisia inaelezwa kuwa kweli mwigizaji huyo ana tatizo hilo.

                      

Hayo yamefichuliwa hivi karibuni na waigizaji wenzake Antony Starr na Chace Crawford walipokuwa kwenye mahojiano ya moja kwa moja na 'Podcast ya Happy Sad Confused' na kudai kuwa mkali huyo ana tatizo la kusinzia kama alivyocheza kwenye filamu. 

                       

Fahamu kuwa 'Narcolepsy' ni tatizo linalosababisha mtu kulala bila mpangilio, hata katika mazingira yasiyofaa. Kama alivyocheza Black Noir, hata hivyo katika mahojiano hayo Antony Starr na Chace Crawford walieleza walivyoweza kuingiza tatizo katika uhalisia wa muhusika na jinsi lilivyoweza kusaidia kuunda scene ambazo zinaacha kumbukumbu kwa watazamaji.