Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vitu wanavyovizingatia Mabantu kabla ya kolabo

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwananchi mmoja wa wanachama wa kundi hilo, Twaah Kane (Mabantu) amesema wao hawaangalia sana umaarufu bali wanazingatia heshima, kipaji na mengineyo.

Dar es Salaam. Kundi maarufu la muziki wa Bongo Fleva nchini, Mabantu ambao kwa sasa wanatamba na ngoma ya ‘Vibaya’ waliyoshirikishwa na msanii wa Singeli Dogo Elisha, wameweka wazi misingi wanayoizingatia katika kufanya kolabo na wasanii wengine.

Akizungumza na Mwananchi mmoja wa wanachama wa kundi hilo, Twaah Kane (Mabantu) amesema wao hawaangalia sana umaarufu bali wanazingatia heshima, kipaji na mengineyo.

“Inategemea msanii yupo kwenye nafasi gani lakini sana ni kipaji na heshima, na tukizungumzia kwa wasanii ambao wapo kwenye nafasi ya juu zaidi basi huwa tunaangalia muunganiko wetu na kitu gani tunataka tukifanye ilikilete maana kwa mashabiki zetu, mtu kama Elisha tuliangalia sana kipaji chake na heshima yake,” amesema

Amesema wao kufanya Singeli kwa sasa sio kwa sababu muziki huo upo kwenye chati bali wameanza kuusapoti kitambo, huku wakiwa na nyimbo zaidi ya nane za muziki huo.

“Kama umeweza kuwafuatilia Mabantu tuliweza kufanya Singeli kipindi ambacho muziki huu haupo hata kwenye chati na kitu kizuri tumebarikiwa sana kwenye muziki huo hatujawahi kufanya Singeli halafu ngoma hiyo ikatuangusha tuna nyimbo takribani nane za Singeli na zote zimefanya vizuri ukiweka na vibaya ya Dogo Elisha, kwa hiyo tumeanza kuithamini Singeli kabla haijapata heshima ambayo inapata, kwa hiyo huu ni muendelezo wa kile tulichokuwa tunafanya kabla," amesema Twaha.

Pia, ameweka wazi kuwa hakukuwa na ugumu wowote kuikamilisha ngoma ya Vibaya kwani Dogo Elisha walitamani kufanya naye kazi muda mrefu.

"Hakukuwa na wakati wowote mgumu na kipindi ambacho tulikuwa tunaandaa 'University Ep', alikuwa ameachia nyimbo yake ya Mr Dj sisi tulikuwa mashabiki wakubwa wa hiyo nyimbo na tulihitaji kuingia kujiunga kufanya naye kazi kwenye wimbo huo, bahati mbaya siku ambayo ilitakiwa tufanikishe hilo tulikuwa na safari ya kuelekea Afrika Kusini hatukufanikiwa kwa hiyo ni mtu ambaye tulihitaji kufanya nae kazi muda mrefu lakini wakati ulikuwa haujafika.

Huwezi amini wimbo wa Vibaya tumefanya kama leo kesho yake tukashuti video siku mbili mbele wimbo huo ukatoka na hakukuwa na ugumu wowote kwa sababu wakati wa Mungu ulikuwa umefika," amesema Twaah.

Hata hivyo, amesema kundi la Mabantu hufanya aina tofautitofauti ya muziki hivyo mashabiki wasitegemee kuwaona kwenye Singeli peke ake.

"Sisi sio wasanii wa Singeli, lakini muziki huo ndio nembo ya taifa kwa sasa hivi kwa hiyo tutafanya kama Mabantu tunavyohitaji kufanya muziki ambao upo kwenye ramani na vaibu yetu ilivyo muda huo."