Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watu 120 waorodhesha kesi mpya dhidi ya Diddy, apambana kujinasua

Muktasari:

  • Akiongea na waandishi wa habari jana Oktoba Mosi, wakili Tony Buzbee kutoka Texas ameweka wazi kuwa watu 120 wamewasilisha madai ya unyanyasaji wa kingono unaodaiwa kufanyika miaka 20 (miongo miwili) iliyopita huku akisema kuwa ana ushahidi wa picha na video

Marekani, Mkali wa Hip-Hop wa Marekani, Sean “Diddy” Combs anatuhumiwa kuhusishwa katika kesi mpya 120 za unyanyasaji wa kingono zinazotarajiwa kuwasilishwa mahakamani siku 30 zijazo kabla ya kesi zake za awali kuanza kusikilizwa.

Akiongea na waandishi wa habari jana Oktoba Mosi, wakili Tony Buzbee kutoka Texas ameweka wazi kuwa watu 120 wamewasilisha madai ya unyanyasaji wa kingono unaodaiwa kufanyika miaka 20 (miongo miwili) iliyopita huku akisema kuwa ana ushahidi wa picha na video.

“Tutawafichua wale waliowezesha mwenendo huu kwa siri. Tutafuatilia jambo hili bila kujali ushahidi utamhusisha nani, watu wengi wenye nguvu, siri nyingi chafu, timu yangu imekusanya picha, video, na ujumbe wa maandishi. 

“Orodha ni ndefu tayari, lakini kwa sababu ya asili ya kesi hii, tutahakikisha kabisa kuwa tuko sahihi kabla ya kufanya hivyo majina haya yatakushangaza,” Buzbee alisema wakati akiwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari.

Aidha wakili huyo alimtaja mhusika mmoja kuwa ni mtoto mwenye umri wa miaka tisa ambapo Diddy na wengine walimnyanyasa kingono katika studio za Bad Boy Records huko New York City.

Buzbee anadai Diddy alimshawishi mvulana huyo wa miaka 9 kwenda kwenye usaili kwa ahadi ya kumpa mkataba wa muziki, na kisha akamnyanyasa kingono. 

Hata hivyo kwa mujibu wa wakili huyo baadhi ya watu maarufu watajumuishwa kwenye kesi hizo huku akidai kuwa atawashitaki kwa kuhusika au kuujua ukweli na kuukalia kimya.

Hata hivyo mkali huyo anapambana kujinasua kutoka kwenye mikono ya sheria baada ya kukusanya wanasheria mashuhuri kuhakikisha wanamtetea na kupata dhamana ya kutoka mahabusu zikiwa zimepita wiki mbili tangu alipotiwa nguvuni.

Ripoti zinafichua Diddy ameandaa jopo la wanasheria mahiri kuhakikisha wanamtetea kwa kuwasilisha hoja zenye nguvu kisheria ili kumtoa mahabusu kwa dhamana, hilo likiwa ni jaribio la tatu baada ya kugomewa dhamana mara mbili.

Chanzo kinafichua rapa huyo mwimbaji wa wimbo wa I Need a Girl, kilifichua Diddy ameongeza mawakili wawili kwenye timu yake ya wanasheria, Anthony Ricco na Alexandra Shapiro ili kuifanya timu hiyo kuwa na nguvu katika kutimiza lengo la kumtetea kwenye kesi ya jinai inayomkabili.

Imeelezwa Ricco ni moja ya wanasheria mahiri kabisa huko Marekani na Alexandra ndiye mwanasheria msomi anayetamba kwa sasa. Mambo yalivyo ni kwamba Diddy ni kama anaunda timu yake kabambe kabisa ya wanasheria ili kuhakikisha anashinda yanayomkabili.

Diddy alikamatwa huko Midtown Manhattan kwenye hoteli ya Park Hyatt New York, Septemba 16 na kufikishwa mahakamani siku iliyofuatia, alipofunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kingono na unyanyasaji wa kijinsia.

Kukamatwa kwa Diddy kumekuja miezi sita tangu polisi walipovamia kwenye makazi yake huko Los Angeles na Miami katika uchunguzi wao wa masuala ya uhalifu wa kingono.

Rapa huyo alijitangaza kuwa hana hatia kwa mashtaka hayo na mwanasheria wake, Marc Agnifilo, alisema mtayarishaji huyo wa muzuki hana hatia na hakuna cha kuficha. Diddy aligomewa dhamana licha ya wanasheria wake mahiri kabisa kuweka bondi ya Dola 50 milioni na kuomba zuio la wageni wa kike kwenye nyumbani kwake huko Miami kwa kipindi chote cha kesi yake.

Hata hivyo, baada ya malumbano makubwa ya kisheria kati ya wanasheria upande wa mashtaka na watetezi na ndiyo jaji wa Andrew Carter alipokataa kumpa dhamana Diddy kwa sababu za kiusalama za mshtakiwa huyo.

Akiwa katika gereza hilo, awali Diddy aligoma kula kwa hofu ya kuwekewa sumu na hasa kwa sababu amekutana na watu aliwahi kuwa na rekodi nao mbaya alipokuwa uraiani.