Mhariri Mwananchi: Mkakati unahitajika kukabili mfumko wa bei

Muktasari:

  • Mhariri wa Uchumi wa Gazeti la Mwananchi, Julius Mnganga ashauri kuwepo kwa mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na mfumuko wa bei za vyakula unaotikisa katika maeneo mbalimbali nchini.

Dar es Salaam. Mhariri wa Uchumi wa Gazeti la Mwananchi, Julius Mnganga amesema kunahitaji mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na mfumko wa bei za vyakula unaotikisa katika maeneo mbalimbali nchini.

 Ameeleza hayo leo Jumatano Februari 8, 2023 katika mjadala kwa njia ya Twitter (Twitter Space) ulioratibiwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, uliohusu ‘nini maoni yako kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali kukabili mfumuko wa bei.’ Na kushirikisha wakulima, wananchi na viongozi wa Serikali akiwemo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji isivyo na kilevi ulikua kwa asilimia 9.7 katika mwaka unaoishia Desemba 2022 ukilinganisha na ilivyokuwa Desemba 2021.

Ongezeko hilo ni kubwa zaidi ukilinganisha na mfumuko wa asilimia 4.9 mwaka mmoja kabla. Mfumuko huu wa bei unachangiwa zaidi na ongezeko la bei ya vyakula kwa sababu asilimia 28.2 ya bidhaa.

Katika maelezo yake, Mnganga amesema mfumuko wa bei unatokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita vya Ukraine na Urusi, vilivyoithiri mataifa karibu yote ulimwenguni.

Amesema Tanzania sio kijiji imeathirika pia na vita hivyo na kusababisha mfumko wa bei na gharama za maisha kuwa juu, ingawa hali imewanufaisha wakulima ambao wamekuwa na uwanda mpana wa kupanga bei za mazao.

“Sasa yule asiyekuwa na mazao, ndio anapata shida kupata bidhaa hizo.Mtu ambaye ana kipato kidogo anaumia zaidi, kwa sababu gharama nyingine zimepanda kuanzia usafiri wa umma.

“Kiuhalisia mtaani kuna maumivu, lakini hali hii haitaji kuendelea kwa muda mrefu kuna hitaji njia za kiuondoka na na hali hii ili kupungumzia mzigo mwananchi na kumletea ahueni ya maisha,” amesema Mnganga.

Mganga ameishauri Serikali ikae na kufanya mazungumzo na wadau, akisema hali sio nzuri mtaani na hatua hiyo itasaidia kuondokana na changamoto hiyo au kuwapunguzia mzigo wananchi na kuleta ahueni.