Takukuru yaokoa Sh365m Geita

Muktasari:

  • Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeokoa zaidi ya Sh365 milioni mkoani Geita katika miezi mitatu iliyopita kutokana na ubadhirifu, rushwa na dhuluma.

Geita. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeokoa zaidi ya Sh365 milioni mkoani Geita katika miezi mitatu iliyopita kutokana na ubadhirifu, rushwa na dhuluma.

Akitoa taarifa ya utendaji wa robo ya kwanza ya mwaka, mkuu wa Takukuru Geita, Leornad Felix alisema “zaidi ya Sh280 milioni zimeokolewa kutoka kampuni ya Junion Construction pamoja na waajiri wengine ambao walikuwa hawapeleki makato ya watumishi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).”

Nchi nzima, Takukuru imekuwa ikiingilia mikatabainayolenga kulipotezea Taifa mapato au kuwapora wanyonge. (Rehema Matowo)