IGP wa Nigeria ahukumiwa miezi mitatu jela

Inspekta Jenerali (IGP) wa Nigeria, Usman Alkali Baba

Muktasari:

Mahakama kuu nchini Nigeria imemhukumu Mkuu wa Polisi nchini humo kifungo cha miezi mitatu jela kwa kutotii amri ya mahakama.

Mahakama kuu nchini Nigeria imemhukumu Mkuu wa Polisi nchini humo kifungo cha miezi mitatu jela kwa kutotii amri ya mahakama.


Uamuzi huo ulifuatia kesi ya ofisa wa polisi ambaye alifukuzwa kazi mwaka 1992 ambapo ofisa huyo alipinga kustaafu kwake kwa kulazimishwa, na kuachishwa kwake kazi baadaye kulikataliwa kortini.


Mahakama imefikia uamuzi huo Jumanne 29, 2022 kuwa Inspekta Jenerali (IGP), Usman Alkali Baba anatakiwa kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela au kutia amri ya mahakama ya kumrejesha kazini ofisa huyo wa polisi.

Taarifa zinasema kuwa mpaka sasa jeshi la polisi limeshindwa kutekeleza agizo hilo.


Vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti kuwa msemaji wa polisi Olumuyiwa Adejobi alielezea uamuzi huo kuwa "wa kushangaza".


Adejobi alisema kuwa Jeshi la Polisi linasoma hukumu hiyo ili kujua hatua za kuchukua.