Kim, Putin kujadili ushirikiano wa kimataifa Russia

Rais wa Russia, Vladimir Putin akisalimiana na Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un. Picha na Maktaba

Russia. Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un jana usiku Jumanne Septemba 12, 2023 amewasili nchini Russia akitumia usafiri binafsi wa treni.

Kim anatarajiwa kukutana na Rais Vladimir Putin katika eneo ambalo bado halijafahamika, licha ya treni yake kuonekana ikielekea eneo la Kaskazini mwa Jiji la Vladivostok

Rais Kim alianza safari kuelekea Russia Jumapili akitumia treni hiyo inayotajwa kuwa na ulinzi mkali na isiyoruhusu risasi kupenya.

Fununu kutoka idara za ujasusi za Marekani zinasema Marais hao huenda wanatarajiwa kujadili makubaliano ya silaha wakati Russia ikiendelea na vita dhidi ya Ukraine.

Hata hivyo Ikulu ya Russia ya Kremlin ilisema kuwa ziara hiyo itahusu "mahusiano ya nchi mbili, katika nyanja ya kimataifa".

Kim alipokelewa na Waziri wa Maliasili wa Russia, Aexander Kozlov