Ramadhosa ‘aruka’ tuhuma za rushwa

Muktasari:
Rais Ramaphosa anadaiwa kuvunja kanuni ya maadili kwa kutakatisha fedha wakati wa kampeni zake za urais mwaka 2017.
Afrika Kusini. Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amekana kampeni yake ya kugombea urais kuhusika na vitendo vya utakatishaji wa fedha chafu.
Ramaphosa amesema hayo jana Jumapili Julai 21, wakayi akihutubia Taifa kwa njia ya televisheni.
Ramaphosa alikuwa akijibu madai yaliyotolea Ijumaa liyopita na mlinzi wa umma, Busisiwe Mkhwebane ambaye alisema kuwa rais huyo amevunja kanuni ya maadili wakati wa kampeni zake mwaka 2017 kupitia chama tawala cha African National Congress.
Ofisi ya Mkhwebane iligundua kwamba kampeni hiyo, inayoitwa CR17, imepokea malipo ya rand 500,000 kutoka kampuni ambayo sasa inahusishwa na kashfa ya rushwa.