Taliban wafanya shambulizi la kigaidi Pakistan

Muktasari:

  • Serikali ya Kaskazini Magharibi mwa Pakistani, imesema  wanamgambo wamefanya shambulizi kwenye kituo cha polisi na kuua askari.

Pakistan. Kundi la Taliban nchini Pakistani linalojulikana pia kama Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP), limethibitisa kuhusika na shambulizi lililofanyika usiku wa kuamkia leo Ijumaa.

 
Shambulizi hilo lilitokea katika Wilaya ya Khyber iliyoko Kaskazini Magharibi mwa nchi hio.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka serikalini inasema wanamgambo hao walitumia bomu na bunduki kutekeleza shambulizi hilo.

Taarifa zinasema askari watatu wa kikosi cha usalama waliuawa.

Mkuu wa Polisi wa Wilaya, Imran Khan amewaambia wanahabari kuwa wanamgambo wanne waliokuwa na silaha nzito walifanya shambulio hilo na kusababisha vifo hivyo.

Khan anasema wanamgambo hao walivamia majengo kwa kile alichokiita kuwa ni mashambulizi yalioratibiwa ya kujitoa mhanga.

Aidha, kundi hilo la TTP, katika taarifa yake limedai kuhusika na shambulizi hilo.