Uwekezaji wa China barani Afrika wafunguliwa zaidi

Muktasari:

Serikali kuu ya China imezipa mamlaka serikali za mitaa na mikoa na kampuni zao kuongoza awamu inayofuata ya biashara kati ya Taifa hilo na baadhi ya nchi barani Afrika.

Serikali kuu ya China imezipa mamlaka serikali za mitaa na mikoa na kampuni zao kuongoza awamu inayofuata ya biashara kati ya Taifa hilo na baadhi ya nchi barani Afrika.


Moja ya majimbo yaliyo katikati ya biashara kati ya China na Afrika ni Zhejiang, mkoa wa pwani wa mashariki mwa China wenye kampuni zinazojenga maghala, mbuga za viwanda na miundombinu ya biashara ya mtandaoni katika nchi za Afrika.


Wiki iliyopita, kampuni za China mjini Zhejiang yalitangaza mpango wa kuweka benki miradi 26 barani Afrika yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 8.1 katika jitihada za kuimarisha biashara na bara hilo.


 Miradi hiyo ilijumuisha Yuan bilioni 1 (Dola za Marekani milioni 140) na Zhejiang Gezhi Trading, kampuni tanzu ya Merit Link Group na Zhejiang Yingfan Trading kujenga ghala la nje ya nchi kwa ajili ya Merit huko Algiers, mji mkuu wa Algeria.


Serikali ya jiji la Jinhua ilisema kituo hicho kinatarajiwa kuhudumia shughuli za kampuni hiyo katika Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini na Afrika ya Kati na Kusini.


Makubaliano hayo yalitiwa saini wiki iliyopita wakati wa mkutano wa 2022 wa China (Zhejiang) kuhusu mahusiano ya kiuchumi na biashara ya China na Afrika na wiki ya ushirikiano wa kitamaduni na mabadilishano ya utamaduni kati ya China na Afrika huko Jinhua, mkoani Zhejiang.


 Hafla hiyo ilivutia wajumbe 400 kutoka China na nchi 47 za Afrika.


Lauren Johnston, mtafiti wa China na Afrika katika taasisi ya masuala ya kimataifa ya Afrika Kusini alisema Zhejiang ni miongoni mwa kitovu cha kijimbo cha China kwa ajili ya biashara ndogo na za kati za sekta binafsi (SMEs).


Alisema pia ni nyumbani kwa Yiwu, kituo cha bidhaa za walaji ambacho kilivutia mamia ya maelfu ya wafanyabiashara wa ndani na mtandao kutoka kote Afrika na Mashariki ya Kati.


"Zaidi ya hayo, kampuni kubwa ya biashara ya mtandaoni Alibaba na taasisi yake ya kimataifa ya kukuza biashara ya kidijitali, Jukwaa la Biashara la Kielektroniki la Dunia (eWTP), walikuwa na makao yake mjini Zhejiang, yenye vituo vya eWTP nchini Ethiopia na Rwanda," alisema Johnston.


Yun Sun, mkuu wa mpango wa China wa kituo cha Stimson mjini Washington alisema Zhejiang alikuwa na historia ndefu ya kusukuma mbele ushirikiano wa kiuchumi na Afrika.


"Kwa kuzingatia majaliwa ya viwanda ya Zhejiang na kipaumbele chake cha biashara ya nje, hii haipaswi kushangaza," alisema.


David Shinn, mtaalam wa uhusiano kati ya China na Afrika katika Chuo Kikuu cha George Washington cha Elliott School of International Affairs, alisema mikoa ya China ina historia ya kushirikiana na nchi nyingine, hasa katika biashara, uwekezaji, elimu, utalii na utamaduni.


 "Beijing imehimiza mawasiliano haya lakini inadhibiti sera ya kigeni," Shinn alisema.


Shinn alisema Zhejiang imekuwa hai  barani Afrika na Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal kinaongoza katika ushirikiano wa elimu kama msingi wa taasisi ya mafunzo ya Afrika na kimetoa mafunzo kwa zaidi ya wanafunzi 8,000 wa Afrika.


"Zhejiang ina mpango wa kubadilishana utalii na Zimbabwe, Tanzania, na Ethiopia," alisema.


"Ikiwa mazoezi ya zamani ni dalili, sio miradi yote hii itafanyika, lakini inawakilisha uwekezaji mkubwa. Lengo kuu la ushirikiano wa majimbo mengi ya China barani Afrika ni kupata faida," alisema.


Katika ripoti ya hivi karibuni iliyoandikwa na shirika la ushauri la Development Reimagined lenye makao yake makuu Beijing, Baraza la Biashara la China na Afrika (CABC) lilisema Zhejiang imepitisha utaratibu wa maingiliano "chini" ili kukuza ushirikiano kati ya China na Afrika kwa ushiriki mkubwa wa vikosi vya kiraia, ikijumuisha kampuni binafsi, vituo vya huduma, taasisi za utafiti na vyumba vya biashara vya ndani.