Wabunge Uingereza wakumbuka mauaji ya Kashmiri Pandit

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Baadhi ya wabunge nchini Uingereza, wahindu na washirika wao wameadhimisha miaka 33 ya mauaji ya halaiki ya Pandits ya Kashmiri.

Dar es Salaam. Baadhi ya wabunge nchini Uingereza, Wahindu na washirika wao wameadhimisha miaka 33 ya mauaji ya halaiki ya Pandits ya Kashmiri.

Tukio hilo lilifanyika nje ya ukumbi wa Bunge mjini London na kuongozwa na Bob Blackman, mwenyekiti wa wabunge wa vyama vyote, kikundi cha APPG cha Wahindu wa Uingereza.

Mapema iliwasilishwa hoja ya kuadhimisha mauaji ya kimbari ya wanaharakati wa Kashmiri iliyotiwa saini na wabunge wa vyama mbalimbali, kuwakumbusha kwamba haki bado haijatendeka.

Bob Blackman alisisitiza uungaji mkono wake kwa India na jamii ya Wahindu wa Kashmiri na kukumbusha kuwa ni uvamizi wa Pakistan wa Kashmir.

Oktoba 26, mwaka 1990  huko Baramullah watu 11,000 waliuawa na wavamizi huku  Maharaja Hari Singh akiomba uingiliaji wa silaha kutoka India ili kutuliza hali na kukandamiza uvamizi huo ambapo Jeshi la India lilisafirisha wanajeshi wake hadi mjini Kashmir na kuzima uvamizi huo ndani ya wiki mbili.

Akizungumza tukio hilo mbunge wa Jonathan Lord amesema, ‘’kama vile tunavyopaswa kusahau kuhusu mauaji ya halaiki, hatupaswi kusahau mauaji haya ya Kimbari.’’

Mbunge Theresa Villiers alituma ujumbe wake kusomwa katika hafla hiyo, “Ulimwengu lazima uelezwe kuhusu dhuluma kubwa iliyofanywa dhidi ya Wahindu wa Kashmiri. Miaka 33 baada ya wengi kufukuzwa kutoka kwa nyumba zao, ni wakati wa kubadilisha simulizi la Kashmir ili sauti ya Wahindu iweze kusikika hatimaye. Nimejitolea kufanya hivi na nasikitika kutoweza kujumuika nanyi kwenye hafla yenu jioni ya leo.”

Wahindu huko Jammu na Kashmir waliteswa na kulazimishwa kukimbia nchi yao mwaka 1989-1990 ambapo  miaka 33 baadaye, mauaji yaliyolengwa kwa Wahindu yanatajwa kuwa bado yanaendelea.