Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi kushirikishwa mchakato wa kumng’oa Gachagua

Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua

Muktasari:

  • Bunge la Kenya limeanza mchakato wa kumng’oa Naibu Rais, Rigathi Gachagua kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya Ofisi. Oktoba 8, 2024 atapaswa kujitetea kwa muda wa saa mbili (sawa na dakika 120).

Nairobi. Spika wa Bunge la Kitaifa la Kenya, Moses Wetang’ula ametangaza ushiriki wa umma katika hoja ya kumng’oa madarakani Naibu Rais, Rigathi Gachagua Ijumaa, Oktoba 4, 2024.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Standard, mchakato huo utafanyika katika kaunti zote 47 na Katibu wa Bunge atatoa taarifa kamili kupitia matangazo ya vyombo vya habari kuanzia leo Jumatano Oktoba 2, 2024.

Wetang'ula amebainisha kuwa shughuli zote za Bunge kuanzia Alhamisi, Oktoba 3, 2024 hadi Jumatatu Oktoba 7, 2024 zitasitishwa ili kupokea maoni ya umma.

Kamati ya Shughuli za Bunge itaweka azimio la kuahirisha kikao cha Bunge kesho Alhamisi na kufanya kikao cha asubuhi Jumanne, Oktoba 8, 2024 kujadili hoja hiyo.

Gachagua anaweza kujitokeza ana kwa ana au kupitia uwakilishi wa kisheria.

Hatua hiyo inafuatia baada ya Mbunge wa Kibwezi Magharibi, Mwengi Mutuse kuwasilisha rasmi hoja ya kumtimua Gashagua, akisema hoja za kufikia uamuzi huo ni sahihi na zinajitosha kumwondoa ofisini.

Wetang'ula alisoma hoja hiyo Jumanne Oktoba Mosi, 2024 na kuthibitisha kuwa wabunge 291 waliiunga mkono hoja hiyo, na kuvuka idadi ya wabunge 117 wanaohitajika ili kuunga mkono hoja hiyo.

Mutuse alitoa waraka wa kurasa 100 za ushahidi zinazoelezea sababu zake za kutaka kiongozi huyo atimuliwe.

“Ibara ya 145 (1) ya Katiba inatamka kwamba mjumbe wa Bunge akiungwa mkono na angalau theluthi moja ya wabunge wote, anaweza kutoa hoja ya kushitakiwa kwa Rais au naibu wake kwa sababu ya ukiukwaji wa Katiba,” amesema Wetang'ula.