Adaiwa kumuua baba yake akimtuhumu mshirikina

Friday June 11 2021
ushirikina pic

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Urlich Matei.

By Hawa Mathias

Mbeya. Mkazi wa wilayani Mbarali mkoani Mbeya , Daniel Manga (30) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji ya baba yake mzazi Victor Manga (79) akimtuhumu kuwa mshirikina.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Urlich Matei alliwambia waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Mei 19 mwaka huu na baada ya kmsako wa polisi walifanikiwa kumtia nguvuni.

Kamanda Matei alisema kuwa mtuhumiwa alimuua baba yake kwa kumkata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha mauti yake kutokana na damu nyingi kumwagika. “Mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu baba yake kuwa ni mshirikina na hivyo kujichukulia uamuzi wa kumkata kwa mapanga kichwani mpaka umauti ukamkuta na tulipomuuliza alikiri, hivyo atafikishwa mahakamani wakati wowte ushahidi ukikamilika”alisema.

Aidha Kamanda Matei ameonya wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kufanya mauaji ya watu wasio na hatia na badala yake watoa taarifa katika vyombo husika ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Mkazi wa Jijini hapa, Saumu Ally aliomba Jeshi la polisi kuwachukulia hatua kali na kutowafumbia macho watu wanaohusiaka na mauaji ya wazazi wao kwani kitendo hicho ni kuwanyima haki ya kuishi wazazi.

Advertisement