Diamond, Harmonize ndani ya MTV 2021

New Content Item (2)
Diamond, Harmonize ndani ya MTV 2021

Muktasari:

Wakali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz, Harmonize, Zuchu n kuindi la Rostam wametajwa kushindania tuzo za MTV 2021, huku Mond akitengenezwa kipengele kipya kwa ili kumtunuku msanii aliyepiga shoo kali kipindi dunia ipo katika lockdown.

Wakali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz, Harmonize, Zuchu n kuindi la Rostam wametajwa kushindania tuzo za MTV 2021, huku Mond akitengenezwa kipengele kipya kwa ili kumtunuku msanii aliyepiga shoo kali kipindi dunia ipo katika lockdown.

Katika kipengele hicho kilichopewa jina la kimombo la Alone Together, Diamond ameingia kutokana na utumbuizaji wa kibunifu zaidi alioufanya kwenye tamasha la kuchangia familia zilizokumbwa na athari za janga la Covid-19, tamasha lilikofanyika Mei mwaka huu na kupewa jina la Africa Day Benefit Concert.

Harmonize ameteuliwa kipengele cha Msanii Bora wa Kiume, huku Zuchu alkiteuliwa kama Msanii anayechipukia, Rostam ikiwa ni Kundi Bora la Muziki, wakati Mond akiingia vipengele viwili, Msanii Bora wa Mwaka na Shoo Kali kipindi cha Lockdown.

Tuzo za MTV Mama zinazotarajiwa kufanyika Uganda mapema mwakani zikiwa na zaidi ya wasanii 30 kutoka nchi 15 za Afrika, huku kwa mara nyingine tena, wasanii kutoka Nigeria wakitawala kwa kutokea mara 14 kwenye vipengele vya tuzo hizo.

Majina ya washiriki wa tuzo hizo zenye vipengele 10 yalitangazwa usiku wa kuamkia Desemba 10 ikiwa ni pamoja na kufungua rasmi pazia kwa mashabiki kuanza kuwapigia kura wasanii wanaowapenda, ambapo kura hizo zinapigwa kupitia tovuti ya mtvmama.com.

Tuzo za MTV Mama zilianzishwa mwaka 2008 maalumu kwa ajili ya wanamuziki wa Afrika na kila mwaka taifa moja kutoka barani humo hupewa kibali cha kuwa mwenyeji. Kwa Afrika Mashariki ni Kenya na Uganda waliowahi kupata kibali hicho.