Kamati ya Bunge yaeleza kusuasua mradi ujenzi nyumba

Kamati ya Bunge yaeleza kusuasua mradi ujenzi nyumba

Muktasari:

  • Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imesema katika ujenzi wa mradi wa nyumba za Dungu ulioanza mwaka 2014 ni nyumba 99 ndio zimekamilika kati ya 439 zinazotakiwa.

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imesema katika ujenzi wa mradi wa nyumba za Dungu ulioanza mwaka 2014 ni nyumba 99 ndio zimekamilika kati ya 439 zinazotakiwa.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Aprili 13, 2021 bungeni mjini Dodoma na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Najma Giga wakati akitoa maoni na ushauri wa kamati hiyo kuhusu mapendekezo ya mapato na matumizi ya wizara zilizo chini ya ofisi ya waziri mkuu.

Giga amesema nyumba 344 zilizobaki ujenzi wake upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na  99 zilizokamilika zimepangishwa kwa watu mbalimbali kwa pango la Sh250,000 na  Sh400,000 kwa mwezi.

"Nyumba hizo zilipangwa kuuzwa kwa bei kati ya Sh132 milioni hadi Sh498 milioni lakini hadi sasa hakuna nyumba iliyouzwa kinyume na matarajio ya
mpango wa mradi," amesema Giga.

Kwa mujibu wa kamati hiyo, walibaini kuwa uwekezaji uliofanywa katika mradi huo umeanza kuwa na manufaa kidogo angalau kwa kuwapangisha watu mbalimbali na kuwezesha makazi ya viongozi wa Wilaya ya Kigamboni.