Dk Mwinyi awataka Wazanzibar kushiriki sensa 2022

đź”´#LIVE: Rais Dk Mwinyi akitoa hutuba ya maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi

Muktasari:

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amewataka Wazanzibar kushiriki katika sense ya watu na makazi inaayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti 2022.

Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amewataka Wazanzibar kushiriki katika sense ya watu na makazi inaayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti 2022.

Dk Mwinyi ametoa wito huo Jumanne Januari 11, 2022 usiku Ikulu ya Zanzibar wakati akitoa hotuba ya kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar zitafanyika katika Uwanja wa Amaan kesho Jumatano.

Dk Mwinyi amesema kuwa maandandalizi yanaenda vizuri hivo wananchi washiriki katika sense hiyo ili kusaidia Serikali kuweza kupata takwimu sahihi kwaajili ya mipango ya maendeleo.

“Ndugu wananchi moja kati ya mambo muhimu tuliyoyafanya mwaka 2021 ni matayarisho ya sense ya wau na makazi ya mwaka 2022, hadi kufikia Desemba 2021 matayarisho hayo yalikuwa wamefikia asilimia 65 ambapo zoezi la majaribio lilifanyika mwezi Septemba 2021 katika maeneo 10 Unguja na Pemba na kazi ya uchambuzi inaendelea” amesema Rais Mwinyi nakuongeza

“Natoa wito kwa wananchi sote, tuhakikishe tunashiriki zoezi hilo wakati litakapofanyika kwa kutoa taarifa sahihi ili tuweze kupanga na kutekeleza mipango yetu ya maendeleo kwa uhakika na ufanisi Zaidi” amesema

Dk Mwinyi anmebainisha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja, changamoto na matarajio ya Serikali hiyo.

Amesema kuwa miongoni mwa mambo ambayo yanafurahisha wakati Zanzibar ikiadhimsha miaka 58 ya Mapinduzi ni kuendelea kuimarika kwa Muungano.

“Wakati nchi yetu ikiadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi, tunafurahia kuendelea kuimarika kwa Muungano wetu wa Tanzania kwa kufanikiwa kudumisha ushusiano wetu wa kihistoria na wadamu kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano” amesema