Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mapadri, bruda waliofariki ajalini kuzikwa Julai 17

Gari aina ya Mitsubishi Outlander ikiwa imepata ajali eneo la Mtualonga mkoani Lindi baada ya kugonga shimo na kupoteza mwelekeo.

Muktasari:

  • Mapadri hao ni Cornelius Modoe (55) wa jijini Dar es Salaam, Pius Boa (51) mkazi wa Tanga na Bakanja Mkenda (51) ambaye ni bruda mkazi wa Dar es Salam. Walifariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea jana Ijumaa Julai 12, 2024 mkoani Lindi.

Mtama. Miili ya mapadri wawili na bruda waliofariki dunia katika ajali gari inatarajiwa kuzikwa Jumatano ijayo Julai 17, 2024 katika makaburi ya Ndanda yaliyopo Kanisa Katoliki mkoani Mtwara.

Watatu hao walifikwa na mauti asubuhi ya jana Ijumaa ya Julai 12, 2024 katika eneo la Mtualonga barabara ya Masasi- Mnazi Mmoja katika Halmashauri ya Mtamaa, Mkoa wa Lindi.

Mapadri hao ni Cornelius Modoe (55) wa jijini Dar es Salaam, Pius Boa (51) mkazi wa Tanga na Bakanja Mkenda (51) ambaye ni bruda mkazi wa Dar es Salam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori alisema gari hilo lilipofika maeneo ya Mtualonga liligonga shimo na kupoteza mwelekeo upande wa kulia na kuacha njia kisha kutumbukia kwenye shimo la karavati na kusababisha vifo na majeruhi wawili.

Miili yao ilihifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Nyangao katika Halmashauri ya Mtama huku majeruhi wawili wakipatiwa matibabu hospitalini hapo.

Leo Jumamosi, Julai 13, 2024, Padri anayewasimamia watawa katika Kanisa Katoliki la Narunyu, Halmashauri ya Mtama, Antony Chilumba amesema miili ya wapendwa wao itazikwa Julai 17, 2024 makaburi ya Ndanda misheni ambayo ni sehemu maalumu wanayozikiwa watawa.

Padri Chilumba amesema siku hiyo wataanza kwa misa takatifu saa 4 asubuhi kwa ajili ya kuwaombea marehemu hao na itakapomalizika misa watawapumzisha kwenye nyumba ya milele.

Aidha amesema majeruhi Bruda Edmund Kimario ameruhusiwa jana na yupo kwenye nyumba ya watawa iliyopo Ndanda. Bruda huyo aliumia sehemu ya mkono lakini dereva Juma Makota bado amelazwa hosptali hapo kwa matibabu zaidi.

"Bruda Edmund ameruhusiwa licha ya kuumia mkono wa kulia lakini anaendelea vizuri,  kwa ndani wamemuwekea chuma, yupo nyumba ya watawa Ndanda kwa uangalizi endapo atapata changamoto yoyote basi iwe rahisi kumpeleka hosptali ya Rufaa ya mkoani Mtwara, na dereva bado amelezwa HospItali ya Nyangao na hali yake inaendelea vizuri leo anaweza kuruhusiwa," amesema Padri Chilumba.

"Mimi nimemjua Padri Mdoe zaidi ya miaka miwili, alikuwa mtu safi sana, waumini wengi walimpenda kwa ukaribu na ushirikiano wake, lakini Bruda Bakanja yeye alikuwa ndiye anayeshughulikia mambo yote kwenye ukatoliki.

Ukitaka kwenda nje ya nchi yeye ndiye anayeshughulikia hati ya kusafiri, mizigo inayotoka nje au inayokwenda nje yeye ndiye mshughulikiaji kiukweli tumepata pengo Wakatoliki wote," amesema Chilumba.