Mrithi wa Chalamila atua ofisini Mwanza

Friday June 11 2021
awasili pic

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila akikabidhi nyaraka kwa Mkuu wa Mkoa huo, Robert Gabriel ikiwa ni makabidhiano ya Ofisi hiyo. Picha na Mpiga picha wetu.

By Mgongo Kaitira

Mwanza. Mkuu  wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel leo Ijumaa Juni 11, 2021 amewasili jijini Mwanza kwa ajili ya makabidhiano ya ofisi na mtangulizi wake, Albart Chalamila ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

 Amefika katika ofisi za mkuu wa mkoa leo saa 4:50 asubuhi na kupokelewa na wajumbe wa kamati ya amani ya mkoa huo.

Kwa mujibu wa katibu mieka wa mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Matia Levi amesema makabidhiano baina ya wawili hao  yanatarajiwa kufanyika wakati wowote leo.

Katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais Samia leo, aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ally Hapi amehamishiwa mkoani Mara kuchukua nafasi ya Gabriel huku aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Batilda Buriani akiteuliwa kuchukua  nafasi ya Hapi.

Advertisement