Profesa Mkenda aipongeza kampuni ya MCL

Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la alizeti unaofanyika mkoani Singida, leo. Kauli mbio ya mkutano huu ni zalisha alizeti kwa uhakika wa mafuta ya kula, kipato na maendeleo ya viwanda. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Waziri wa Kilimo nchini Tanzania,  Profesa Adolf Mkenda ameipongeza Kampuni ya Mwananchi Communications Limited  (MCL)  kwa kutenga kurasa kwenye magazeti yake kwa ajili ya habari za kilimo.

Singida. Waziri wa Kilimo nchini Tanzania,  Profesa Adolf Mkenda ameipongeza Kampuni ya Mwananchi Communications Limited  (MCL)  kwa kutenga kurasa kwenye magazeti yake kwa ajili ya habari za kilimo.

 Amesema hayo leo Jumapili Juni 13, 2021 katika mkutano  unaofanyika mkoani Singida unaoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa ajili ya kuzungumzia uzalishaji wa malighafi za mafuta ya kula ikiwamo alizeti, pamba na karanga katika mikoa mitatu ya kielelezo ya Singida, Dodoma na Simiyu.

"Nichukue nafasi ya upendeleo wa pekee kumpongeza ndugu Bakari Machumu ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mwananchi inayochapisha magazeti ya Mwananchi na The Citizen kwa kuamua kuja mwenyewe na timu. Naomba usimame," amesema Waziri Mkenda.

Profesa Mkenda ametoa pongezi hizo kwa Machumu kwenye mkutano huo akisema kazi inayofanywa na MCL na hasa kwa kuja na timu kwenye mkutano huu ni ya kupongezwa.