Rais Samia azindua kiwanda cha kusafisha dhahabu

Sunday June 13 2021
samia dhahabu pic
By Mgongo Kaitira

Mwanza. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumapili Juni 13, 2021 amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Mwanza Precious Metal Refinery (MMPR) kilichojengwa kwa  Sh12.2 bilioni.

Kiwanda hicho kilichojengwa na Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kwa kushirikiana na Kampuni ya Lozera ya nchini Dubai kina uwezo wa kusafisha kilo 480 za madini kwa siku.

Hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho imehudhuriwa na wakazi wa Jiji la Mwanza, viongozi wa Serikali, kisiasa na kidini.

Mtendaji mkuu wa kiwanda hicho, Anand Mohan ameishukuru Serikali kwa kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho huku akisema kitachangia kukuza uchumi wa Tanzania.


Advertisement