Serikali kujenga tuta Jangwani

Tuesday April 13 2021
jangwani pc
By Habel Chidawali

Dodoma. Serikali imesema ipo katika mchakato wa kujenga tuta kubwa katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam ili kuondoa kero kwa wananchi inayotokana na kujaa maji kila mvua kubwa inaponyesha.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Aprili 13, 2021 bungeni mjini Dodoma na naibu waziri wa Tamisemi, David Silinde na kufafanua kuwa shughuli ya kuimarisha miundombinu katika eneo hilo inafanyika.

Silinde alikuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum,  Agnes Kaiza aliyehoji lini Serikali itamaliza kero ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam hasa eneo la Jangwani.

Naibu waziri huyo amesema Serikali imeweka mkakati wa kumaliza kero hiyo kwa kujenga miundombinu itakayopitisha maji ili yasituame na kuwa kero.

Katika swali la msingi mbunge wa Viti Maalum,  Tunza Malipo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kumaliza kero ya maji kwa wananchi wa Mtwara Mikindani ambapo iliwapimia na kugawa viwanja maeneo ambayo yanajaa maji.

Akijibu swali hilo, Silinde amesema Serikali inatengeneza mkakati maalumu wa kuhakikisha inajenga miundombinu imara ya kuondoa matatizo hayo.

Advertisement
Advertisement