Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

163 mbaroni kwa tuhuma mbalimbali Njombe

Muktasari:

  • Watuhumiwa 163 washikiliwa mkoani Njombe kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo wizi wa Bajaji na Pikipiki.

Njombe. Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa wapatao 163 kutokana na tuhuma mbalimbali za uhalifu ikiwemo wizi wa bajaji na pikipiki.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Banga wakati akizungumza na waandishi wa habari hapa mkoani Njombe.

Amesema makosa mengine yaliyosababisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni pamoja na uporaji, uvunjaji na mauaji ya watu.

Amesema msako uliofanywa na jeshi hilo kuanzia mwezi Septemba 1 mpaka 31 Oktoba 2023 ndiyo umefanikisha kukamata watuhumiwa hao pamoja na Bajaj, Pikipiki na vifaa vinginevyo.

Amesema jeshi hilo limekamata Bajaji zipatazo nane, Pikipiki tatu, matairi ya Bajaji sita, dizeli lita 328, bangi gramu 200, simu pamoja televisheni.

Amewataka madereva wa Bajaji mkoani Njombe kuhakikisha kuwa wanawafahamu abiria wanaowabeba na mazingira wanayoenda ili kuepuka uporaji wa Bajaji hizo.

"Kumekuwa na tabia ya watu kukodiwa na kupelekwa maeneo hatarishi ambayo wanakwenda kunyang'anywa Bajaji lakini jeshi limeendelea kufanya doria na kuwasaka wanaojihusisha na uporaji wa Bajaji" amesema Banga.

Amesema katika msako huo jeshi hilo limemkamata Stephano Mng'ong'o (55) baada ya kukutwa na silaha moja aina ya gobole ambayo alikuwa anaimiliki kinyume cha sheria.

Mwenyekiti wa madereva wa Bajaji Wilaya ya Njombe, Richard Luganga amesema wizi wa Bajaji umesababisha mgongano mkubwa kati ya madereva na wamiliki wa Bajaji mkoani Njombe.

"Kwa madereva imezua taharuki basda ya kuona vile vyombo ambavyo wao wanatumia kutafutia riziki vinatoweka katika mazingira ambayo hayaeleweki" amesema Luganga.

Mmoja ya madereva wa Bajaji mkoani Njombe Geofrey Mwinuka amesema Bajaji zilizo nyingi zinaibiwa muda wa kuanzia saa tano mpaka saa nane usiku.

"Bajaji nyingi zinaibiwa sehemu tunayopaki hasa sehemu ambazo siyo salama kwani kwenye ulinzi mzuri Bajaji haziibiwi," amesema Mwinuka.